Baada ya kuachia single mpya aliyowashirikisha wasanii wa kimataifa Ms Triniti na Lamyia wa Marekani, Ambwene Yessaya aka AY anatarajia kuachia video mbili kwa mpigo mwezi ujao (October).
AY amesema video moja itakuwa ni ya single yake mpya ‘Its Going Down’ ambayo audio yake ameiachia wiki iliyopita, na ya pili ameamua iwe ‘surprise’ kwa mashabiki wake lakini zote zitafanyika Miami, Marekani.
“Nitachomoa mashine mbili, videos. So ni surprise kwenu…hapa niko kwenye mchakato wa kufanya video na baada ya video nauhakika tutaendelea kupeperusha bendera ya muziki wa Bongo au East Africa kwa ujumla.” alisema kupitia The Jump Off ya Times Fm.“So la msingi ni hivyo, October video inatoka ‘It’s Going Down’ na video nyingine ambayo ni surprise kwenu.”
No comments
Post a Comment