Detroit Pistons huenda ikamchukua Hasheem Thabeet lakini...

Hasheem 2
Hasheem Thabeet anadaiwa kuwepo kwenye roaster ya mazoezi ya timu ya kikapu ya Detroit Pistons ambayo huenda ikamsaini kwa mkataba usiokuwa na ‘guarantee’.
Taarifa hiyo ni kwa mujibu wa ESPN.
Thabeet ameichezea Oklahoma City Thunder kwa misimu miwili kabla ya kuuzwa kwa Philadelphia 76ers ambao walimwacha huru. Hata hivyo sio rahisi kwa Thabeet kuanza kuichezea Pistons pale msimu wa kawaida utakapoanza kwakuwa tayari timu hiyo ina wachezaji 16 wenye mikataba yenye guarantee.
Ili aweze kucheza, ni lazima waachie au kuwauza wachezaji wawili na tayari timu hiyo ina mchezaji mwenye umbo kubwa kama lake, Aaron Gray katika benchi. Bado haijafahamika iwapo Thabeet ana nafasi ya kucheza kwenye NBA tena, lakini kama atatokea mara nyingi kwenye kambi ya mazoezi anaweza kupata nafasi.
TAG