HII NDIYO MAANA YA NDOA / MAHUSIANO!.


Kiukweli kabisa mchepuko siyo dili kwa kuwa wengi waliochepuka wamejikuta kwenye matatizo makubwa sana. Ndiyo maana tunashauriwa kubaki njia kuu kwa kujenga uaminifu kwa wale tuliotokea kuwapenda na kutodiriki kuwasaliti. Lakini wakati ukweli ukiwa hivyo, kasiya kusalitiana kwa wapenzi imekuwa ikiongezeka kila kukicha. Utulivu umekuwa sifuri, unayedhani katulia kesho utasikia kafumaniwa.Unaweza kuwa na mpenzi ambaye kila mara anakueleza kuwa, hawezi kukusaliti na atakuwa na wewe katikashida na raha lakini huyohuyo usishangae siku moja ukamkuta yuko na mtu mwingine.Swali la kujiuliza ni kwamba, kwa nini wapenzi wanashindwa kujizuia na mchepuko? Hivi hawaoni hatari iliyopo mbele yao kwa kuwasaliti wenza wao? Mimi nadhani kuna tatizo lakini hebu tuone sababu ambazo zinaonekana kuwasukuma baadhi ya wanandoa kushindwa kutulia kwenye njia kuu.Katika utafiti niliofanya nimebaini kuwa, tamaa za kijinga zimekuwa zikisababisha wengi kuwasaliti wenza wao na kuwasababishia maumivu makubwa sana.Tamaa hasa ya pesa imekuwa ikiwashawishi baadhi ya watu kushindwa kujizuilia kusaliti. Kwa wale ambao wako kwenye ndoa wakati mwingine hasa wanawake wasipopatiwa mahitaji yao muhimu na akatokea jamaa, akamhakikishia kupata kila anachotaka, anakubali bila kujua kwamba anakosea.Wengine wanapatiwa kila kitu na waume zao lakini sasa kinachotokea ni tamaa za kimwili tu ambazo zinawasumbua na kujikuta wanatafuta wanaume wengine huku wakidai kuwa wanatafuta ladha tofauti.Lakini wengi wamekuwa wakichepuka kutokana na mazingira wanayojengewa na wenza wao.

TAG