Msanii wa muziki wa asili nchini, Mrisho Mpoto anatarajia kuachia wimbo mpya mwezi ujao. Wimbo huo umetengenezwa na producer Alan Mapigo katika studio zake mwenye Mpoto.
Akizungumza na Bongo5 leo, afisa habari wa Mpoto Theatre Gallery, Dominic, alisema wimbo Ndovelwa ni wimbo wa asili kama kawaida yake ambapo ndani ya wimbo huo amemshirikisha msanii mkubwa wa hapa nchini.
“Mpoto yupo kwenye tour ya masuala ya afya huko mikoani ila kikubwa ambacho amewaandalia mashabiki wa muziki wake ni wimbo ‘Ndovelwa’ mwezi wa kumi. Pia huu wimbo ameshirikishwa msanii mkubwa, mambo mengine mengi wadau wasubiri watakuja kuona tu,” amesema Dominic.
No comments
Post a Comment