Mbunge wa Mbeya Mjini, Joseph Mbilinyi aka Sugu ameachana na aliyekuwa mchumbake Faiza Ally.
Wawili hao wana mtoto wa kike. Faiza amethibitisha kuachana na Sugu kwenye Instagram kwa kushare pia ya pamoja.
“Mtoto wangu wa Faiza na Joseph ana fikisha miaka 2 kesho , nimeangalia kumbu kumbu zangu na baba yake toka mimba yake mpaka leo nimejikuta nalia sana nalia kwa furaha na lia kwa uchungu mkali mno nalia kwa furaha kwa sababu nimefurahi kuwa nae katika maisha yangu sana , hakuna kitakacho nipa furaha hapa duniani Kama kumuona Sasha anakua na afya furaha anapata elimu nzuri na maisha mazuri na anapata elimu ya dini na ya duniani na zaidi kumjua mungu# nalia kwa uchungu mkali kwa sababu ndoto zangu mimi na baba yake ilikua tumlee pamoja na tumuangalie kwa macho yetu mpaka mwisho wa maisha yake .. Lkn haiko hivyo .. Hii inauma sana jamani kuachana na baba wa mtoto hasa mtoto akiwa ktk umri mdogo uchungu ninao uasikia Sasa hivi hauna maelezo NINAUMIA sana sana sana nalia kwa nguvu mno wazazi jamani nawasihi hasa wanaume msiache wake zenu au wazazi wenzetu wanawake tunaumia sana yaani hata ukijitahidi vipi kila unapo muona mtoto lzm utamuona na baba yake naumia sioni aibu kusema hili NAUMIA Lkn mwisho was siku sina cha kufanya nashukuru kwa yote maana haya ndio maajaliwa yangu nataka tu kuwaambia wazazi ambao mko kwenye ndoa na ambao hampo kwenye ndoa Kama mna watoto vumilianeni na mrekebishe tofauti zenu ili watoto wenu wawe ktk malezi ya wazazi wote Wawili …. NAWAPENDA WATOTO WOTE na wamama single Kama mm pamoja na yote Lkn jitahidi tuwalee watoto wetu na tuwapenda muda wa kutosha na sisi ili wasione sana upweke wa kukosa baba kwa karibu … Love yupo the single mother duniani.”
No comments
Post a Comment