Fainali za Dance100% kutimua vumbi Jumamosi hii.

001.Dance












Meneja wa Uhusiano wa Umma wa Vodacom Tanzania, Matina Nkurlu (kulia) akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam jana juu ya fainali ya mashindano hayo yatakayofanyika jumamosi Don Bosco Oysterbay jijini. Kulia ni Mratibu wa shindano hilo la Dance 100%, Happy Shame
FAINALI za shindano la kucheza muziki maarufu kama Dance 100% linalofanyika chini ya uratibu wa Kituo cha East Africa Television ltd na kudhaminiwa na kampuni ya mawasiliano ya Vodacom Tanzania, zitanayika Jumamosi hii ya Oktoba 4, Viwanja vya Don Bosco, Oysterbay jijini Dar es Salaam.

Mratibu wa shindano hilo Happy Shame alisema jijini Dr es Salaam jana kuwa, fainali za shindano hilo ambalo safari yake ilianza Julai 19, mwaka huu kuanzia hatua ya kusaka washiriki hadi mchujo litashirikisha makundi matano.
Alisema kutokana na kila kundi kutaka kuibuka mshindi na kujitwalia kitita cha shilingi mil 5, kwa muda mrefu yamekuwa yakijifua kuhakikisha wanafanya kweli siku hiyo mbele ya jopo la majaji wakiongozwa na Super Nyamwela.
Shame alisema, shindano la mwaka huu limekuwa na msisimko wa aina yake zaidi kuliko miaka miwili iliyopita baada ya mambo mbalimbali kuboreshwa na zaidi kiasi cha vijana kuona ni fursa kwao sio tu kupata fedha, pia kuendeleza vipaji vyao. “Ushindani umekuwa mkubwa sana katika shindano la mwaka huu ikilinganishwa na miaka mingine kutokana na sababu mbalimbali. Shindano pia limeanza kupata mashabiki, tunashukuru sana sapoti ya wadhamini wetu Vodacom Tanzania,” alisema.
Kwa upande wake Meneja Uhusiano wa Umma wa Vodacom Tanzania, Matina Nkurlu,alieleza kuwa mbali ya dau hilo kwa mshindi, kila mshiriki pia atapatiwa simu iliyounganishwa na mtandao wa Vodacom. Nkurlu alisema jana kuwa, kundi litakaloibuka nafasi ya pili katika fainali hiyo, litajipatia zawadi ya sh Milion 1.5 na mshindi wa tatu atapata kiasi cha laki 5.
Alisema kampuni ya Vodacom inajivunia kudhamini shindano hilo kwa njia hiyo yaudhamini wakitambua umuhimu wa vijana kujiajiri kupitia vipaji vyao na kuongeza kuwa, kwa kipindi chote cha mchakato wa shindano hilo, vijana wamejifunza mengi. “Vijana wameonyesha uwezo mkubwa kuanzia hatua ya mchujo hadi sasa kiasi cha kuwapa
majaji wakati mgumu. Tunaamini hata baada ya fainali, vijana hawa watajiendeleza zaidi kimuziki,” alisema Nkurlu.
Makundi hayo matano yaliyoingia hatua ya fainali, vijana wamekuwa wakionesha vipaji na umahiri mkubwa wa kucheza staili mbalimbali za muziki ambayo ni Wazawa Crew, Best Boys Crew, The W.T, Wakali Sisi na The winners Crew. Nkurlu aliongeza kuwa, kwa vile vijana hao wamejiweka katika mazingira ya kutumia vipaji vyao kujipatia ajira, Kampuni ya Vodacom-Tanzania inaona fahari kudhamini shindano hilo wakisaidia juhudi za serikali kupambana na tatizo la ajira.
“Takwimu zinaonesha kuwa kila mwaka vijana zaidi ya 800,000 wanaingia katika soko la kusaka ajira ndio maana, Vodacom Tanzania kwa kulitambua hilo, tumekuwa mstari wa mbele kusaidiana na serikali na wadau wengine kuwajengea vijana msingi,” alisema Nkurlu.
Kuhusu zawadi, Nkurlu alisema kundi litakaloibuka mshindi, litaondoka na shilingi mil 5, huku kila mshiriki katika katika kundi hilo akipatiwa simu aina ya Vodafone ikiwa na muda wa maongezi wa shilingi 100,000.
TAG