“Hivi karibuni nilikuwa na Wema, nimemwambia aongee na Diamond ili tufanye filamu ya pamoja,” amesema Majuto. “Mimi, Wema na Diamond, hata Diamond ninaweza kuzungumza naye sema nimeanza na Wema kwanza, akikubali mtasikia tu.”
Kwa upande mwingine Majuto amesema ili acheze filamu anahitaji kulipwa shilingi milioni 3.
“Umri unaenda sasa biashara za nisaidie nisaide hakuna, kama unanitaka ili tufanye kazi unatakiwa uandae milioni 3.”
No comments
Post a Comment