MOVIE: TAKEN 3 MOVIE TRAILER

Liam Neeson anarejea tena kwenye muendelezo wa tatu wa filamu ya Taken. Awamu hii baada ya Liam anayejulikana kama Bryan Mills kwenye filamu hii, anajikuta kwenye wakati mgumu muda mfupi baada ya kurudiana na mke wake ambaye anauawa nyumbani kwake.

Anajikuta akidhaniwa kuwa ndiye aliyehusika kwenye kifo hicho na hivyo anakimbia na kutafutwa kwa udi na uvumba na CIA, FBI na polisi. Kwa mara ya mwisho, Mills anatakiwa kutumia ujuzi wake kuwatafuta wauaji halisi wa mke wake na pia kumlinda binti yake mpendwa. Filamu hiyo inaingia kwenye majumba ya sinema January 6, 2015.
TAG