Mwenyekiti wa bunge maalum la katiba Samuel Sitta amewaonya watu wanaoupinga mchakato wa kupata katiba mpya kuacha kutumia njia za vitisho kwa baadhi ya wajumbe wa bunge hilo na kuupotosha umma juu ya mwenendo wa mchakato huo.
Mh. Sita alitoa onyo hilo jana asubuhi bungeni mjini Dodoma na kueleza kuwa kuna watu wasiojulikana wamewatishia kwa ujumbe wa simu baadhi ya wajumbe wa bunge maalum la katibawanaoendelea na mchakato huo.
Amesema baadhi ya wajumbe kutoka Zanzibar walionesha jumbe hizo kwa uongozi wa bunge hilo maalum na kuomba kuondoka mjini kwa kuhofia usalama wao na wakaruhusiwa.
Aidha Mh. Sitta amewataka viongozi wa dini wasitoe maagizo ya masuala ya siasa kwa kutumia nyumba za ibada.
Wajumbe wa bunge maalum la katiba ambao hawakupata fursa ya kushiriki zoezi la kuipigia kura rasimu ya katiba inayopendekezwa na bunge hilo lililoanza mwanzoni mwa juma hili, leo wamepiga kura
No comments
Post a Comment