Snoop Dogg amesainishwa na label Pharrell Williams. Mtandao wa Billboard umesema album ijayo ya Snoop itatoka chini ya label hiyo, i am OTHER pamoja na Columbia Records.
Pharrell atatayarisha album nzima ambayo wasanii watakaoshirikishwa ni pamoja Stevie Wonder na Charlie Wilson. Kwenye interview na Big Boy, Pharrell alisema album hiyo ni kama imeshakalimika na kwamba ni kali kuzidi hata ya yake mwenyewe.
Wawili hao wamewahi kufanya kazi kadhaa pamoja ikiwa ni pamoja na hit ya Snoop ya mwaka 2003, ‘Beautiful’ na ile ya mwaka 2004, ‘Drop It Like It’s Hot.’
No comments
Post a Comment