Paris Hilton atumia shilingi milioni 379 baa, aingiza bilioni 4.4 kwa udj wa siku 4.

1411756456660_Image_galleryImage_10_AUGUST_2014_SAINT_TROP
Paris Hilton hivi karibuni ametumia $230,000 ambazo ni takriban shilingi 379,500,000 kunywa pombe na marafiki zake.

DJ Paris Hilton
Mrembo huyo na washoga zake walitumia $100,000 peke yake kununua chupa kubwa za Ace of Spades Champagne na chupa 11 kila moja za Patrón, Cristal na Grey Goose, kwa mujibu wa mtandao wa Page Six.
1411755287055_wps_14_Paris_Hilton_looks_fabulo
Kutokana na bili hiyo, Paris alitoa tip ya $47,000 kwa wahudumu wa kiota hicho ambayo ni zaidi ya shilingi milioni 77. Kwa Hilton, hiyo si fedha ya kuwaza kwakuwa anadaiwa kuingiza dola milioni 2.7 ambazo ni zaidi ya shilingi bilioni 4.4 kwa kucheza tu muziki kama DJ kwa siku nne.
Tags