Rich Mavoko amesema haikuwa kazi rahisi kukubali kukaa karibu na yule mnyama cheetah anayeonekana kwenye video ya wimbo wake mpya ‘Pacha Wangu’.
Mavoko ameiambia Bongo5 kuwa awali aligoma kabisa. “Haikuwa rahisi aisee,” amesema Mavoko. “Nakumbuka wakati tumefika pale, hali ilibadilika ghafla cause plan ilikuwa ni kwamba cheetah apigwe shot za peke yake akiwa anatembea, lakini Adam akabadilisha script, akasema ‘Mavoko inabidi uimbe na cheetah’. Mwanzo niligoma kabisa, ila baada ya kunishawishi yeye na yule mama wa kizungu anayemfuga, ambaye akanipa mifano akaniambia ‘mbona akina Burner Boy na Dbanj walishoot naye bila kuogopa you can do it too’ ndo nikajikaza kisabuni ikabidi nikubali. Ila haikuwa rahisi kwasababu yule cheetah ni wa kweli na ana meno, ila nashukuru Mungu tulipata shot nzuri.”
Chini ni video ya wimbo wa Burna Boy ‘Don Gordon’ ambamo cheetah huyo anaonekana pia.
Watanzania wengi wa nje na ndani ya nchi wamempongeza Rich Mavoko kwa video nzuri iliyoshootiwa jijini Cape Town, Afrika Kusini.
No comments
Post a Comment