Video: Kanye na Kim waajiri walinzi wenye silaha baada ya kushambuliwa jijini Paris.

1411727137547_wps_70_25_Sep_2014_PARIS_FRANCE_
Kim Kardashian akisongwa na umati mkubwa wa watu.
Licha ya kuwashangaza watu wengi kwa nguo zao walizovaa wakati wa Paris Fashion Week, sasa itakuwa ngumu zaidi kuwasogelea au kuwagusa Kanye na mke wake Kim.
Kim Kardashian, 33, na Kanye West, 37, wanadaiwa kuwa na wasiwasi mkubwa baada ya kushambuliwa wakiwa red carpet na mwandishi wa habari wa zamani, Vitalii Sediuk kiasi cha kutaka kumwangusha chini Kim.
1411727260359_wps_75_25_SEPT_2014_PARIS_FRANCE
Wakati mrembo huyo alipokuwa akitoka kwenye gari kwenda kumshuhudia mdogo Kendall Jenner, 18, akishiriki kwenye show hiyo, Vitalii anadaiwa kumvuta nywele Kim huku Kanye na mama yake wakishuhudia.

Kutokana na tukio hilo, Kim na Kanye wamedaiwa kuajiri walinzi wenye silaha za moto watakaokuwa wakimlinda muda wote akiwa Paris.
Wanandoa hao wametengeneza headlines jijini humo kwa aina ya nguo wanazovaa.
1411726939551_Image_galleryImage_PARIS_FRANCE_SEPTEMBER_25
1411727738901_Image_galleryImage_Kanye_West_and_Kim_Kardas

Tags