Dully Sykes na Spice Digital vitani, asema wamemdhulumu, wao wasema wanamdai.

10012439_937781559572246_2072180109_n

Msanii mkongwe nchini, Dully Sykes amefunguka kwa uchungu na kusema kuwa yupo kwenye muziki miaka 15 lakini bado hajanufaika na kitu chochote kupitia muziki. Hivi karibuni msanii huyo ameingia kwenye vita vya maneno na kampuni ya Spice Digital ambayo anadai imemdhulumu pesa zake za mauzo ya RBT ya mwaka mzima.
Dully ameitaka kampuni hiyo kumlipa pesa zake zote na kuvunja naye makataba baada ya kuona wamekuwa sio waaminifu.
“Nimeshadhulumiwa sana kwakweli, na sasa hivi nina miaka 15 kwenye muziki sioni faida yoyote, najiona nipo nipo tu,” Dully ameiambia Bongo5. “Naimba kama msanii basi lakini sio msanii mwenye maendeleo tena na pesa zangu zipo kwa watu bado nawadai. Nimeifikisha bongoflava mbali lakini bado thamani yangu haijulikani iko wapi! Mimi sitaki tena mambo ya caller tune, kwa sababu wanaiba sana. Kampuni ya Spice imenifanya kitu kibaya sana, kwasababu sioni faida yake. Maisha yangu yanaenda vizuri tu. Mwaka jana walikuwa wananilipa milioni moja kwa kila mwezi na pia walikuwa wananikopesha kama nahitaji kukopa, sasa mwaka huu sijachukua hata mia na kila nikiwatafuta wanatupiana mpira. Huu sio ugomvi, mimi ninachoweza kusema wanipe pesa zangu tuvunje mkataba basi, sitaki kuendelea kuwa nawanenepesha kwa kazi yangu, tuvunje mkataba waendelee kufanya kazi na wasanii wengine,” alisema Dully.
Kwa upande wake msemaji wa kampuni hiyo Michael Mlingwa aka MX amesema Dully haidai fedha yoyote.
“Dully hakuna hela ambayo anadai, sisi ndo tunamdai yeye,” amesema MX. “Hii kampuni imeingia makataba na Dully, Dully akitaka kuondoka kwenye kampuni hawezi kwenye vyombo vya habari, anatakiwa atutumie barua ya kutuambia madai yake, hakuna anayemkataza. So anachofanya sasa hivi anakosea. Mwaka ulioisha tulikuwa tunampa milioni moja kwa kila mwezi ameuza hajauza, so ile ilikuwa ni minimum guarantee. Kampuni inavyompa vile tunatakiwa tuje kurecover kwenye pesa zake za mauzo. Kama mauzo yake ni laki 3 halafu tumempa milioni moja, maana yake kuna laki 7 ambayo kampuni imempa Dully. Mwaka mwingine unapoanza tuangalia hali ya utafiti mwaka ulioisha. Sasa haya ni makubaliano yote ambayo alisaini mkataba, sasa kwa sababu yeye ameongea sisi tuna vithibitisho vya mkataba,” aliongeza MX.
Pia MX amesema endapo Dully atavunja mkataba atachukuliwa hatua za kisheria kwakuwa kampuni bado inamdai.
“Kama anataka kuvunja mkataba anatakiwa atoe damage ya mkataba alioingia, kwasababu kampuni imeingia hasara, na hiyo damage anatakiwa atutumie barua ya kuvunja mkataba sisi tutaangalia tunavunja naye mkataba kwa sababu gani? Kama report zake tukiangalia itakuwa rahisi kulizungumza, tumeshamtumia mpaka email kuhusu login zake kwa sababu report zote zipo online. Kwahiyo anatakiwa kutuma barua, akishatuma barua tutaangalia ni tatizo gani linalomfanya avunje mkataba.”
TAG