Mr Blue: Young Killer ni bonge moja la Rapper!

Mr BlueRapper Mr Blue amemmwagia misifa msanii kutoka Mwanza, Young Killer Msodoki na kudai kuwa alikuwa haamini kama ni yeye ndiye anayetunga mistari ya nyimbo zake.
Akizungumza na Bongo5 leo, Mr Blue amesema maneno anayotoa rapper huyo hayalingani na umri wake kwakuwa yanaonyesha ukomavu mkubwa.
“Kiukweli huwaga siamini yeye ndio anatunga mistari anayoimba, dogo anaweza sana,” amesema. “Kwasababu mistari anayotunga inazidi umri wake. Unajua wakati namsikia Young Killer nilikuwa sijawahi kuonana naye. Time nakutana naye ilikuwa kwa Mona nikamtuma kitu fulani, baadaye baada ya kukaa nikaambiwa yule ndo Young Killer baada ya kumfutilia nikaona Young Killer Msodoki ni msanii mkubwa sana, ni rapper mzuri sana,”amesema Blue.
Hata hivyo Blue amemshauri Killer ufanyia mazoezi matamshi ya maneno.
“Tatizo lililopo kwa dogo ni kwenye lugha ambalo kwa sasa hivi ameanza kulifanyika kazi. Ukiangalia huwaga wanasema rapper ni msemaji mkuu kwahiyo ukiangalia vizuri ni lazima ujue kusema vizuri.”
Kwa upande mwingine Blue amesema kuongezeka kwa rapper wadogo wadogo kumaanisha muziki umekua.
“Muziki upo sehemu mbili unaweza ukawa mgumu na unaweza ukawa rahisi. Professor Jay naye aliwahi kusema.. kwa sababu wao ndo malegend wa muziki huo kwa sababu mimi nimekuwa nikimsikiliza Jay nyimbo kama Chemsha Bongo, nilikuwa nikizichana zile ngoma kwahiyo ninachoweza kusema ambacho Jay mwenyewe alisema, unapoona underground wengi wanakuja it means biashara ya muziki imeanza kukua.”
“Kwahiyo mimi nataka nitoe tu ushauri kwa hawa rappers ambao wanakuja kuwa rap ni kujitolea, kama umetaka kuwa rapper jitolee kufuatila rappers wengine, lugha kwenye matamshi. Unaweza kukuta mtu rapper mkubwa lakini kwenye lafudhi neno rafiki anasema ‘lafiki’, sasa unamfundisha nini mtu anayekusikiliza/ Kwahiyo tujifunze kuwa ma-rapper wanaojua lugha na wanasema maneno adimu ambayo mtu yatamfundisha na kumburudisha pia. Huo ndio ushauri wangu,” amesisitiza Kabayser.
TAG