Licha ya Sean Kingston kutoza gharama kubwa kwa watu wanaotaka kufanya nae collabo, lakini mzee wa commercial Ambwene Yessaya a.k.a AY amesema hadi sasa amesharekodi nae mara tatu bila kumlipa pesa yoyote.
AY ameiambia Bongo5 kuwa kipaji ndio kilichopelekea kupata nafasi ya kufanya nae wimbo, licha ya kuwa Sean huwatoza watu wengine dola 30,000 kufanya nae collabo.
“Hajawai kunilipisha, talent yako ndio inakubeba sometimes” amesema AY. “Unajua ukiweka hela mbele kwaajili ya kufanya collabo na watu, inakua talent yako ndo inabebwa na hela, usipokuwa na hela hamna kitu tena. So mi nachofanya naitumia talent yangu. Kwanza inaanza ushkaji inafata talent, ikija talent sasa kunakua kuna kitu wanaita unajenga nae trust..”
“ingawa watu wengine wakienda wanaambiwa dola elfu 30 kurekodi nae, sio mchezo, na mimi namwingiza studio mara ya tatu, unajua mi nina ngoma nae mbili, inagawa moja hatukuifurahia hivyo tukasema hii haitatoka.”
AY ambaye anatarajia kuachia collabo hiyo aliyofanya na Sean Kingston mwezi ujao (November) amesema hivi sasa wamekua marafiki wa karibu sana.
“sometimes yeye unakuta alienda studio yupo na kina Omarion kwenda kuangalia ngoma yangu imemixiwaje, ananiambia oya tupo hapa na kina Omarion jamaa wanafurahia kazi nini, ukija next time tunaweza kuonana nao vitu kama hivyo huwezi jua anakutengenezea daraja la kwenda sehemu nyingine zaidi. Kwahiyo mi siaminigi kulipa hela ili kufanya collabo no, sijawahi kufanya hivyo, kwasababu hata mi mwenyewe mpaka nikubali collabo na mtu naangalia talent.”
Akizungumzia collabo hiyo ambayo imekaa muda mrefu bila kutoka tangu aanze kuizungumzia amesema,
“November naitoa…unajua track yangu na Sean tulibadilisha tena , yaani unajua wimbo huwezi kukaa nao muda mrefu vile kwahiyo inabidi mrekodi tena, kwahiyo tumebadilisha badilisha baadhi ya sehemu, yaani imekuwa tofauti na vile kama mwanzo ilitakiwa itoke.“
“November naitoa…unajua track yangu na Sean tulibadilisha tena , yaani unajua wimbo huwezi kukaa nao muda mrefu vile kwahiyo inabidi mrekodi tena, kwahiyo tumebadilisha badilisha baadhi ya sehemu, yaani imekuwa tofauti na vile kama mwanzo ilitakiwa itoke.“
No comments
Post a Comment