Filamu maarufu ya, vmpires, Twilight inatarajia kurejea kwenye mfumo wa filamu fupi tano zitakazooneshwa kupitia mtandao wa Facebook.
Waongozaji watano wa kike watachaguliwa kutengeneza filamu zao fupi zinazotokana na kitabu cha “The Storytellers – New Creative Voices of The Twilight Saga”.
Waongozaji hao watafundishwa na kundi la wataalam akiwemo muigizaji wa “Twilight” Kristen Stewart na mwandishi wa vitabu hivyo, Stephenie Meyer. Filamu hizo ni sehemu ya mradi Women in Film, Lionsgate na Facebook unaolenga kuwapa uwezo wanawake kutumia ubinifu wao.
No comments
Post a Comment