Kanye West kufanya wimbo wa pamoja na mkewe Kim Kardashian

Kanye na kim
Rapper Kanye West pamoja na mke wake Kim Kardashian ambaye kwa pamoja wanatarajia kupata mtoto wao wa pili, wanadaiwa kuwa na mpango wa kuingia studio kufanya collabo!
Chanzo kimoja kimeliambia gazeti la The Sun kuwa Kim ameamua kuanza kujifunza kupiga piano kama sehemu ya maandalizi ya collabo hiyo, na kuwa Kanye ana mpango wa kuachia wimbo huo mara tu baada ya mke wake kujifungua mtoto wao wa pili.
Kim aliwahi kujaribu kuimba mwaka 2011 aliporekodi wimbo uliokuwa ukiitwa Jam (turn it Up) ambao baadae alikuja kukiri kuwa anajuta kufanya jaribio la kuimba kwa sababu aligundua sio fani yake!
“It’s definitely a memory and it was a fun experience. But if there’s one thing in my life I wish I didn’t do … I don’t like it when people kind of dabble into things they shouldn’t. And that I don’t think I should have….Like, what gave me the right to think I could be a singer? Like, I don’t have a good voice.” Alisema Kim K.
Sikiliza wimbo wa Kim Kardashian alioutoa mwaka 2011
TAG