Hard Blasters waingia studio kurekodi ngoma za ‘come back’, Professor Jay asema wataachia single 2 ‘soon’

HBCBaada ya ahadi za muda mrefu za kurudi kwa kundi la Hard Blasters, rapper Joseph Haule a.k.a Professor Jay amethibitisha kuwa HBC inatarajia kufanya ‘come back’ kwa kuachia ngoma mbili mpya kwa mpigo hivi karibuni.

Hard Blasters (Prof Jay, Fanani na Big Willy)
Prof Jay ameiambia Bongo5 kuwa HBC tayari wameingia studio na kuanza kurekodi kazi mpya zinazotarajiwa kutoka hivi karibuni.

“Jana tumeingia studio kwaajili ya kuanza mavurugu vurugu, watu wategemee mabalaa makubwa sana muda si mrefu, kwahiyo Hard Blasters tumeirudisha sio tumeirudisha Hard Blasters inakuja kivingine so watu wategemee vitu vikubwa.“
Tarajia kuisikia HBC iliyokamilika kwa kuwasikia wote Professor Jay, Fanani na Big Willy.“Tumehusika wote watatu (Jay, Fanani na Willy), production tumeifanya pale Mwanalizombe producer ni Villy ndo tunaanza nayo hivyo.”
Jay pia amepost picha akiwa na Fanani na Willy na kuandika“HARD BLASTERS ndani ya Mwanalizombe studios jana…. Natumaini nimejibu maswali ya watu wengi sana…Stay tuned Kwa MZIGO MZITO sana!!!!”
Jay na Fanani
Katika post nyingine aliandika,“#KAZI KAZINI #HBC at Mwanalizombe studios With my Nigga FANANI Jana Usiku! !! Stay tuned. .. Balaa linakuja @villydavid.”
Jay amesema HBC inakuja na projects nyingi lakini kwa sasa wanaanza na single mbili,
“Kwa kuanzia lazima tuanze na project lazima tuanze na singles na vitu kama hivyo, watu wakae tayari kwa single mbili zinaweza zikatoka muda si mrefu ambazo zitakuwa zinahusisha mambo mengine mengine kwenye jamii,lakini project zinafuata zaidi na zaidi…Kitu ambacho tulikuwa tunawaambia watu kila siku ni kwamba Hard Blasters iko pale sema time tu tunaisubiri ambayo inaweza ikatufanya tukaendelea kufanya kazi pamoja. So kutokana na watu kuwa busy Fanani akiwa na shughuli zake huku na kule, Willy nae alikuwa busy lakini tumeona kilio cha watu wetu kimekuwa kikubwa kwahiyo tumeona kama tuwape wanachostahili.”
TAG