Young Killer: Nisingekuwa msanii basi ningekuwa shehe au mchezaji.

Young Killer akiwa na mpenzi wake Halima pamoja na rafiki yao
Young Killer akiwa na mpenzi wake Halima pamoja na rafiki yao
Kama asingekuwa rapper, Young Killer Msodoki angekuwa shehe anayeswalisha msikiti au mcheza kabumbu.
Young Killer amesema muziki kwake umekuja tu na sio kitu alichotegemea kufanya.
“Kiukweli kabisa mimi nilikuwa najua nakuja kuwa mchezaji na sio msanii,” rapper huyo ameiambia Bongo5. “Nisingekuwa shehe, ningekuwa nchezaji. Yaani shehe, mchezaji au msanii, ila sana sana usanii ilikuwa haipo. Nilikuwa nilikuwa ni mtu ambaye narap home home si unajua zile! Lakini vitu ambavyo nilikuwa nimevishikilia sana na nilikuwa naamini vitakuja kunitoa ni kuwa shehe au kuwa mchezaji mpira,” ameongeza Msodoki.
10684167_292510097621109_1239437494_n
Pia Msodoki ambaye ni shabiki wa timu ya Yanga amefunguka ya moyoni juu ya machungu ya timu yake inapoteza mchezo.
“Kuanza kuishabikia timu ya Yanga nimeanza nikiwa na kama miaka 10 fUlani hivi. Yanga ni timu yangu kitambo na inapofungwa naumia sana hasa tukifungwa na Simba hiyo siku kwangu itakuwa mbaya na nitalala mapema sana kwa sababu nakosa raha kabisa.”
TAG