Muigizaji wa filamu nchini, Salma Tamim maarufu kama Sabby Angel, ameweka wazi uhusiano wake na aliyewahi kuwa mwakilishi wa Tanzania kwenye shindano la Big Brother Africa ‘Stargame’, Julio Batallia.
Sabby ambaye ameigiza kwenye filamu kadhaa za Bongo Movie zikiwemo ‘Moto wa Radi’, ‘Hard Price’, ‘Siri ya Giningi’ na zingine ameweka wazi uhusiano huo kupitia Instagram kwa kupost picha akiwa na Julio ambaye pia ni rapper.
“Am so in love with this man.. am still in love… i dont care that he doesnt feel the same.. i dont care that haters talk shit.. we are not together but i will always love him and i swear to never love again,” ameandika Sabby kwenye moja ya picha akiwa na Julio.
Pamoja na kuigiza, Sabby pia ni muimbaji na pia ataonekana kwenye video ya wimbo wa TID na Jay Moe, Chumvini
No comments
Post a Comment