Peter Msechu aelezea furaha aliyoipata baada ya kutajwa kuwania tuzo (AFRIMA) kwa mara ya kwanza.

Picha MsechuMwimbaji Peter Msechu ameelezea furaha yake baada ya kutajwa kuwania tuzo za kimataifa za ‘All African Music Awards’ 2014 (AFRIMA) za Nigeria (Ingia hapa), ambazo majina ya wanaoshindanishwa yalitangazwa wiki iliyopita.
Msechu ambaye ametajwa kuwania tuzo hizo pamoja na Diamond na Vanessa Mdee, amesema kuwa ameweka rekodi katika historia yake ya muziki kwa kuwa hajawahi kutajwa kuwania tuzo yoyote.
“Sijawahi kutegemea hata kuingia Music Kili Awards lakini unatoka nyumbani unaruka tambo mbili unadondokea Nigeria, laah leo siogi ndugu yangu… Siwezi kuoga sababu naona nimeamka na nuksi moja ya hatari nuksi ya heri” alielezea furaha yake kupitia 255 ya XXL wiki iliyopita.
“Aisee bana nina furaha ya ajabu sana kukiweli yaani sikuwahi kutegemea yaani kwa haraka haraka, kuna wasanii ambao wako kwenye level flani ambao wanapigana na hizo tuzo unajua level flani za juu sana ambao hizo ndo tuzo zao wakina Diamond wakina nani tunawasikia kila kukicha,tulishazoea lakini mtu kama mimi nimeishia kuperform tu kwenye Music Kili Awards kama performer lakini hata kutajwa kama nominee hapa bongo haijawahi kutokea, sasa leo hii ndugu yangu naingia kwenye category kama hiyo halafu watu ninaoshindana nao Kidumu, Jose Chameleone, Diamond mwenyewe sijui kina nani nani eti Best East African artist aah ni hatari”.
Msechu ambaye ameingia kwenye tuzo hizo kupitia wimbo wake wa ‘Nyota’, alikumbushia kauli aliyowahi kuitoa wakati anatoa wimbo huo alioshirikisana na Amini kuwa usingefanya vizuri angeacha muziki, na kudai kuwa alijua kuwa wimbo huo utampa mafanikio.
“Kiukweli nastahili kwasababu kama unakumbuka nilitangazaga kauli moja nilisemaga kama Nyota isipofanya vizuri naacha muziki, lakini nilitangaza ile kauli nilikuwa namaana kubwa kwasababu nilijkua nimeshaiaminia sana nyimbo yangu ya nyota. Kumbuka nyimbo yangu ya Nyota ni nyimbo ambayo imetoka baada ya mimi kusemwa sana, naimba miziki migumu, nafreestyle sana, siumbi melody, sifanyi chochote.”
Alimaliza kwa utani kuwa licha ya kuwa hii ni mara yake ya kwanza kutajwa kuwania tuzo rasmi lakini…“Nilishakuwa nominated sana lakini nanominatiwa hapa hapa nyimbani na mke wangu anani nominate bwana utashinda tuzo nyimbo bora, video bora sina video umeelewa, lakini tuzo as tuzo official tuzo hii ni mara yangu ya kwanza kwahiyo naandika historia kunominatiwa nje ya nyumbani.”
Naye Diamond aliongea na Bongo5 kuhusu furaha yake ya kutajwa kuwania tuzo hizo.
“Kusema za ukweli na furaha sana kuchaguliwa tena katika hizi tuzo za AFRIMA. Ni furaha sana kuona wanajali kile nachofanya maana sapoti yao ndo inafanya watu waone kile ninachofanya. Nawashukuru sana na. Pia Namshukuru sana Mungu kwa kunifungulia njia hizi. Pia nimefurahi zaidi kuona safari hii nipo na Watanzania wenzangu maana ilikuwa ikiniumiza sana kuona nachaguliwa peke yangu tu kila siku. Unajua kama hivi mnakuwa wawili halafu wote mnatoka nchi moja inakuwa ina nguvu zaidi hata kuzungumza kuliko ile unakuta upo peke yako tu. ila mkiwa kama hivi inatia moyo sana.”
TAG