Happy Birthday Diamond: Mmanyema mwenye uchaga kipesa, uhaya kisifa na uzungu kikazi.

10666280_304619959745459_704373199_nKwa mujibu wa meneja wake Babu Tale, Diamond ni mmanyema mwenye uchaga kipesa, uhaya kisifa na uzungu kikazi.
“Acha niseme hili tangu siku tunakutana mpaka leo haujawai kukosa kunipa shikamoo ni ishara ya heshima ya kweli na sio ya kuigiza,” ameandika Tale kwenye ujumbe wa kumpongeza staa huyo kwenye siku yake ya kuzaliwa, Oct 2.
Staa huyo anafanya bonge la party kujipongeza leo na pia ametoa nafasi chache kwa mashabiki wake kuhudhuria.
“Najua wote tungependa tufurahie kwa pamoja siku yangu hii ya kuzaliwa, lakini kwa bahati mbaya hakuna ukumbi utaoweza kututosheleza… sasa tafadhali naomba niambie, unahisi ni kwanini nikupatie wewe kadi hii ili uwe muwakilishi wa Mashabiki zangu??? (nataka nitoe kadi kwa watu 5),” ameandika kwenye ukurasa wa Facebook.
Diamond anasherehekea siku yake ya kuzaliwa siku chache tu baada ya ile ya mpenzi wake Wema ambapo alimzawadia gari jipya. Kupitia Instagram, Wema ameandika: Happy Birthday to you my original soul… ngoja nitulie kwanza ndo niandike caption maana nina mengi kwa kweli… ila jua nakupenda sana…
TAG