Tatizo la mgao wa umeme nchini linatarajiwa kwisha ifikapo mwezi machi mwaka 2015.
Hatua hiyo itafikiwa kutokana na mtambo unaojengwa katika kituo kingine cha umeme kilichopo Tabata kinyerezi kuongezeka na kitakuwa na uwezo wa kuzalisha umeme mega watts 150.
Akizungumza jijini Dar es Salaam Katibu Mkuu wa wizara ya Nishati na Madini Eliakimu Maswi amesema hadi sasa wana jumla ya vituo kumi ambavyo vinazalisha umeme.
Naye Mkuu wa Mkoa Said Mecky Sadick ametoa wito kwa wanachi kutunza miundombinu ili kusudio lililowekwa katika maendeleo ya nchi hususan katika gesi na umeme liweze kufikiwa kwa wakati.
Serikali imeweza kugharimia mtambo wa umeme katika kituo hicho kilichopo Tabata kinyerezi kwa Dollar million 139 ambazo ni fedha za serikari na sio za ufadhili.
No comments
Post a Comment