Platnumz Diamond atokea kwenye Billboard na Dailymail katika tuzo za MTV EMA

Diamond billboard
Ushindi wa Diamond Platnumz kwenye tuzo za MTV EMA kwenye kipengele cha ‘Worldwide Act Africa/India’ umemuweka mwimbaji huyo wa ‘Nana’ katika level nyingine kabisa kimataifa.
Picha za Diamond kwenye Red Carpet pamoja na jina lake kama mshindi wa kipengele hicho zimepewa nafasi kwenye mitandao mbalimbali mikubwa duniani ikiwemo Billboard.com ya Marekani pamoja na Dailymail.co.uk ya Uingereza.
Tuzo hiyo imemwongezea heshima kubwa mtoto wa Tandale ambaye Watanzania walimshuhudia kukua kwake toka alipotoa wimbo wake wa kwanza ‘Nenda Kamwambie’.
Ingia hapa kusoma kwenye Dailymail
TAG